Mamlaka & Kazi

Mamlaka

Kifungu cha 63 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kimeanzisha Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kama ni chombo cha kutunga sheria, sambamba na Ibara ya 106 na 107 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kama vilivyo baadhi ya vyombo vya kutunga sheria, mamlaka kuu ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ni kushughulikia masuala yasiyokuwa ya Muungano kuhusiana na kutunga sheria, kusimamia utekelezaji wa Serikali na uwakilishi.

Kazi za Baraza la Wawakilishi

Baraza la Wawakilishi la Zanzibar litafanya kazi zifuatazo, kama ilivyoelezwa kwenye kifungu cha 88 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984:

  • (a) Kutunga sheria pale ambapo utekelezaji wa jambo unahitaji kuwepo kwa sheria hiyo;
  • (b) Kujadili shughuli za kila Wizara wakati wa kikao cha mwaka wa Bajeti katika Baraza la Wawakilishi;
  • (c) Kuuliza masuala mbali mbali kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Baraza la Wawakilishi;
  • (d) Kuidhinisha na kusimamia mipango ya maendeleo ya Serikali katika njia ile ile ambayo Bajeti ya mwaka inaidhinishwa.
//