Ziara ya Katibu wa Baraza la Wawakilishi Dodoma.

Posted on: 02.11.2026
Ziara ya Katibu wa Baraza la Wawakilishi
Dodoma.
Katibu wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg. Hassan Ali Haji amekutana na Katibu wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Baraka Ildephonce Leonard katika
ofisi za Bunge Dodoma kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kikazi baina ya
taasisi mbili hizo za Kibunge.
Kukutana
makatibu hao kunadhihirisha umuhimu wa kudumisha uhusiano wa ofisi ya Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar na Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania hasa katika
kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kwa lengo la kuongeza ufanisi katika
kutekeleza majukumu yao.
Katika
mazungumzo yao pande zote mbili zimeonesha umuhimu wa kudumisha uhusiano wa
karibu kwa kuimarisha na kuweka misingi imara ya mawasiliano na kujifunza mbinu
bora za usimamizi na uendeshaji wa shughuli za kibunge.