WIZARA YA TAWALA ZA MIKOA YASHAURIWA KUJENGA MAJENGO YA MAKAO MAKUU.

Posted on: 11.05.2026
Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa
Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeishauri
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ kuandaa
mipango itakayoibua miradi ya ujenzi wa majengo ya makao makuu ya wizara.
Kamati imetoa ushauri huo baada ya Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ kuwasilisha Hotuba ya
Bajeti ya Mapato kwa Mwaka wa fedha 2026/2027 katika Ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi Chukwani.
Kamati imesema kuibuliwa kwa miradi ya ujenzi
kwa wizara hiyo kutasaidia kupunguza changamoto uhaba wa Ofisi na kukidhi mahitaji
ya watumishi.
Aidha Kamati imebaini tatizo la kutoonekana kwa
mapato yaliyopangwa kutoka Hazina kwa mwaka wa fedha 2026/2027 licha ya
kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amewaomba Wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi kuidhinisha matumizi ya shilingi 695,735,989,000/= na mapato ya shilingi 8,817,956,000/= kwa
mwaka wa fedha 2026/2027.