Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 15 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi
Posted on: 13.05.2024
Mkutano wa 15 wa baraza la 10 la Wawakilishi unatarajiwa
kuanza siku ya Jumatano 15/05/2024.
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari kuhusu Mkutano huo,
Mkurugenzi wa Shughuli za Baraza la Wawakilishi ndugu Othman Ali haji
amefahamisha kuwa katika Mkutano huo kutakua na shughuli mbali mbali ikiwemo
maswali na majibu, Majadiliano ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwa mwaka wa fedha 2024 - 2025 na Miswada ya Sheria.