Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 12 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi

Posted on: 11.09.2023

Mkutano wa Kumi na Mbili wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 13 Septemba, 2023, saa 3:00 asubuhi.

 

A: SHUGHULI ZA BARAZA:

 

Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-

 

1. Maswali na Majibu.

Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 116 kwa ajili ya Mkutano huu.


2. 
Ripoti za Wizara zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu utekelezaji wa Maoni, Ushauri na Mapendekezo ya Kamati za Kudumu za Baraza kwa mwaka 2022/2023.3. Ripoti za Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali (PAC) na  Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali za Mitaa na Mashirika (LAAC) za mwaka 2020/2021.


4.  Taarifa ya Serikali Kuhusu Ripoti ya Jitihada za Utekelezaji wa Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar mwaka 2022

//