Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 11 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi

Posted on: 09.05.2023

Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 10 Mei, 2023, saa 3:00 asubuhi.

A: SHUGHULI ZA BARAZA

Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-

1. Maswali.

Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 246 kwa ajili ya Mkutano huu.

2 Majadiliano ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

3. Miswada ya Sheria.

Miswada minne ya Sheria itawasilishwa na kujadiliwa, Miswada yenyewe ni:-

i.             Mswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill)

ii.           Mswada wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2023/2024.

iii.       Mswada wa Kufuta Sheria ya Kuzuiya Rushwa na Kuhujumu Uchumi Zanzibar Nam. 1 ya Mwaka 2012 na  Kutunga Upya Sheria ya Kuzuia Rushwa na Kuhujumu Uchumi Zanzibar na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.

iv.      Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Shirika la Mawasiliano Zanzibar na Kuweka Masharti Yanayohusiana na Huduma ya Miundombinu ya Tehama na Mambo Mengine Yanayohusiana na hayo.

4. Miswada Kusomwa mara ya Kwanza

5. Mengineyo kwa ruhusa ya Mwenyekiti

//