Spika Zubeir aongoza Bonanza Arusha.

Posted on: 02.08.2026

Spika Zubeir aongoza Bonanza Arusha.

Spika wa Baraza la Wawakilishi  Mhe. Zubeir Ali Maulid amesema mabonanza ya michezo ni muhimu katika kujenga Taifa lenye afya, upendo na heshima katika jamii.

Mhe. Zubeir ameyaeleza hayo wakati akifungua bonanza lililowashirikisha Wajumbe wa Baraza hilo na Timu ya Arusha Wazee Sport Club lililofanyika katika kiwanja cha Future Stars Academy jijini Arusha.

Amesema Bonanza hilo ni sehemu muhimu kwa Baraza la Wawakilishi katika kulitumia kama chombo cha kuwaleta Pamoja viongozi na jamii kwa lengo la kudumisha udugu kupitia michezo na kutoa msukumo kwa jamii kwa lengo la kudumisha udugu kupitia michezo na kutoa msukumo kwa jamii katika kuunga mkono michezo.

Washiriki wengine wa Bonanza hilo wamependekeza Bonanza hilo liendelee kuwa kigezo muhimu cha kuunganisha Taifa na kukuza utalii kupitia michezo ili jamii iwe na afya bora.

Bonanza hilo lilijumuisha mechi ya mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta Kamba, mchezo wa bao, mchezo wa viti (chair dancing), mbio za magunia na marathon ya kilomita sita.

//