Mkutano wa kwanza wa Baraza la 11 la Wawakilishi Zanzibar.

Posted on: 06.11.2025

Mkutano wa kwanza wa Baraza la kumi na moja la Wawakilishi Zanzibar umeanza leo siku ya Alkhamis ya tarehe 06 Novemba 2025.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Msellem amesema shughuli kubwa za Mkutano huo ni uchaguzi wa Spika, kiapo cha Mhe. Spika, kiapo cha uaminifu cha Wajumbe wote na Uzinduzi rasmi wa Baraza hilo. 

//