Kuanza Kazi Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi
Posted on: 30.10.2023
Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi
zimeanza Vikao vyake leo tarehe 30 Oktoba 2023, ikiwa ni mzunguko wa Pili wa
kazi za kawaida za Kamati. Vikao hivyo vimeanza Kisiwani Pemba na vinatarajiwa
kuhitimishwa Unguja tarehe 17 Novemba, 2023.
Kamati zinafanya Vikao hivyo kwa
ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Kumi na Tatu wa Baraza la Kumi la Wawakilishi
unaotarajiwa kuanza tarehe 29 Novemba, 2023.
Kamati zilizoanza kazi leo ni Kamati
ya kuchunguza na kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika (PAC), Kamati ya
Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa na Kamati ya Bajeti