Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo ya BLW kutembelea maeneo ya kihistoria Mangapwani.

Posted on: 02.11.2026
Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo
ya BLW kutembelea maeneo ya kihistoria Mangapwani.
Kamati Utalii,
Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeishauri wizara ya
Utalii na Mambo ya kale kuboresha na kuimarisha miundombinu ya maeneo ya
kihistoria ili kuongeza idadi ya watalii watakaotembelea maeneo hayo.
Kamati hiyo
chini ya Kaimu Mwenyekiti Mhe. Said Ali Juma wamesema maeneo ya kihistoria ni
mengi hivyo ni wajibu wa wizara kuyaimarisha na kuyaboresha Pamoja na kutoa
elimu kwa umma kuhusu uwepo wa maeneo hayo.
Wajumbe hao
wamefafanua kuwa wizara inawajibu wa kutumia mitandao ya kijamii pamoja na watu
wenye ushawishi wa kuyatangaza maeneo hayo ya kihistoria.
Waziri wa Utalii
na Mambo ya kale Mhe. Nassra Nassor Omar amesema wizara inaendelea kuchukua
hatua mbalimbali ikiwemo kuwapa mafunzo watendaji wa wizara ili kuboresha
utendaji wa kazi zao.
Kamati ya
Utalii, Biashara na Kilimo ilifanya ziara ya kutembelea maeneo ya kihistoria
ikiwemo kisima cha chini kwa chini na Mahandaki ya watumwa Mangapwani.