HOUSE OF REPRESENTATIVES

BARAZA LA WAWAKILISHI

News from the House

Baraza la Wawakilishi SC yaifundisha Soka NMB

TIMU ya Baraza la Wawakilishi Sports Club inayojumuisha timu ya mpira wa miguu, na kikapu imeibuka washindi na kunyakua vikombe viwili katika bonanza maalum ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya kusherehekea miaka 58 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar lililozikutanisha timu ya Baraza la Wawakilishi na timu ya benki za NMB katika mchezo. 

Timu ya kwanza ya Baraza la Wawakilishi kushinda kikombe ilikuwa timu ya mpira wa kikapu kwa wanaume ambayo iliwafunga wapinzani wao timu ya mpira wa kikapu ya NMB kwa jumla ya vikapu 52 kwa 42.

Kikombe cha pili kwa timu ya Baraza la Wawakilishi kilipatikana kwa timu ya mpira wa miguu ambayo iliwafunga NMB goli  9 kwa 8 kupitia mikwaju ya penanti baada ya kutoka sare tasa ya kutokufungana katika dakika 90 za mchezo huo na kuwafanya baraza la  kuendeleza rekodi ya kufanya vizuri katika  mchezo ya ligi na ile ya kirafiki.

 

Timu ya Baraza la Wawakilishi Sports Club na NMB Sports Club zimekuwa zikikutana zikicheza michezo mbalimbali ikiwa na lengo ya kuboresha uhusiano baina ya Baraza na NMB ambapo kwa mwaka huu bonanza hilo limefanyika katika uwanja wa Mao


Hon. Zubeir Ali Maulid (Speaker)

Upcoming Events