HOUSE OF REPRESENTATIVES

BARAZA LA WAWAKILISHI

News from the House

Naibu Spika aongoza zoezi la Usafi BLW

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma amewaongoza Watumishi na Watendaji wa Baraza la wawakilishi katika zoezi la usafi katika maeneo ya Baraza hilo Chukwani Nje kidogo ya Jiji la Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya kukamilika zoezi hilo Mhe Mgeni amesema ni jukumu la kila Mtumishi kuyatunza na kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguuka ili kuepukana na athari mbali mbali zinazotokana na uchafu ikiwemo magonjwa yanayoweza kuzuilika.

Aidha amesema zoezi la kufanya usafi ni endelevu na amewataka watumishi kujitokeza kwa wingi  pindi wanapotakiwa kufanya usafi.

 

Mapema mkuu wa idara ya shughuli za Baraza na shauri wa sheria Baraza la Wawakilishi Zanzibar ndugu Othman Ali Haji amewashukuru watendaji wa baraza la wawakilishi kwa kuitikia wito huo wa kufanya usafi katika maeneo yao ya kazi na kuwaomba kuendelea na utaratibu huo ili kuweka mazingira yanyovutia katika baraza hilo.


Hon. Zubeir Ali Maulid (Speaker)

Upcoming Events