HOUSE OF REPRESENTATIVES

BARAZA LA WAWAKILISHI

News from the House

BLW lapata Mjumbe Mpya

Baraza la Wawakilishi limetapata mwakilishi mpya kufuatia uchaguzi mdogo wa jimbo la Pandani uliofanyika Machi 28, 2021 baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kumtangaza Profesa Omar Fakih Hamad wa Chama cha ACT WAZALENDO  kuwa mshindi wa Uchaguzi huo  kwa kupata kura 2,361 sawa na asilimia 52.55 %  za kura zote halali 4,500.

Uchaguzi huo umekuja kufuatia aliyekuwa  Mwakilishi  Mteule wa Jimbo la Pandani kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Abubakar Khamis Bakary  kufariki dunia Jumatano ya  tarehe 11 Novemba 2020.

Profesa Omar Fakih Hamad anatarajiwa kuapishwa rasmi kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Jimbo la Pandani katika Mkutano wa Tatu wa Baraza la Kumi la  Wawakilishi  Zanzibar  unaotarajiwa kuanza mwazoni mwa Mwezi wa Mei ambao pia utajadili Bajeti ya Serikali kwa mwaka fedha 2021/2022.

Kupatikana kwa Mjumbe huyo mpya kutalifanya Baraza la Wawakilishi kufikia idadi ya  Wajumbe 77.  Wajumbe wa kuchaguliwa na wananchi kutoka majimboni ni 50, Wajumbe wa Kuteuliwa na Rais ni  7, Wajumbe wa Viti Maalum (Wanawake) ni 18, Mwanasheria Mkuu 1 na Spika 1.


Hon. Zubeir Ali Maulid (Speaker)

Upcoming Events

Stay connected