Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 9 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi

Posted on: 21.11.2022

Mkutano wa Nane wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku
ya Jumatano tarehe 23 November, 2022, saa 3:00 asubuhi.

A: SHUGHULI ZA BARAZA:
Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-

 1. Maswali na Majibu.
  Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 138 kwa ajili ya Mkutano huu.
 2. Miswada ya Sheria.
  Miswada ya Sheria iliowasilishwa na kusomwa mara ya kwanza katika Mkutano wa September 2022, itasomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa katika Mkutano huu wa Tisa , Miswada yenyewe ni:-
  i. Mswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Watu wenye ulemavu (Haki na
  Fursa), Nam. 9 ya 2006 na kuweka masharti yanayohusiana na watu wenye ulemavu na mambo mengine
  yanayohusiana na hayo.
  ii. Mswada wa Sheria ya kurekebisha Sheria ya Chuo cha Utawala wa Umma Nam 1 2007 na mambo mengine yanayohusiana na
  hayo.
 3. Miswada kwa hati ya Dharura.
  • i. Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbali mbali
  • ii. Mswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Bodi ya Mapato na Kutunga Sheria mpya ya Bodi ya Mapato Zanzibar.
 4. Taarifa ya Serikali  Taarifa hii itahusu uwasilishwaji wa Ripoti ya Sita ya Utekelezaji wa kazi za Tume ya Maadili kwa mwaka 2021/2022

//