Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi washiriki mbio za Kili International Marathon

Posted on: 27.02.2023
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
wameungana na wanamichezo kutoka Mataifa mbali mbali katika msimu wa
ishirini na moja wa mbio za Kili International Marathon zilizofanyika
mkoani Kilimanjaro wilaya ya Moshi.
Wajumbe hao wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Sport Club Mhe. Miraji Khamis Mussa
wameshiriki katika umbali tofauti ikiwemo kilomita 5, 21 na 42 yaliyoanzia
katika viwanja vya chuo cha ushirika mkoani moshi.