Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 19 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi

Posted on: 05.05.2025

Mkutano wa Kumi na Tisa wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 07 Mei, 2025, saa 3:00 asubuhi.

A: SHUGHULI ZA BARAZA:

Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-

1.   Maswali na Majibu.

Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 311 kwa ajili ya Mkutano huu.

 

2.   Majadiliano ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

 

3.   Miswada ya Sheria.

Miswada miwili ya Sheria itawasilishwa na kujadiliwa, Miswada yenyewe ni:-

i.             Mswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill)

ii.           Mswada wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2025/2026.

 

4.     Kuvunjwa kwa Baraza la Kumi la Wawakilishi, Zanzibar.

//