Spika awaapisha Wajumbe wawili wapya

Posted on: 16.09.2026
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir
Ali Maulid amewaapisha Wajumbe wapya wawili kufuatia uteuzi wa Mheshimiwa Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi Septemba
14, 2026.
Wajumbe walioapishwa ni Mheshimiwa Nassor Ahmed
Mazrui na Mheshimiwa Omar Said Shaaban wote kutoka Chama cha ACT Wazalendo.
Kuapishwa kwa Wajumbe hao ni Hatua muhimu inayowapa
nafasi ya kuanza kutekeleza majukumu yao rasmi ndani ya Baraza, ikiwemo
kushiriki katika mijadala na shughuli mbalimbali zinazohusu maendeleo na
masuala ya wananchi wa Zanzibzr.
Kuapishwa kwa Wajumbe hao kunakamilisha idadi ya
Wajumbe 82 kwa mujibu wa kifungu cha 64 cha Katiba ya Zanzibar toleo la 2020.
Idadi hiyo imetokana na Wajumbe 50 kutoka Majimboni,
20 nafasi maalum za Wanawake (Special seat), nafasi 10 za Uteuzi wa Mheshimiwa
Rais, nafasi 1 ya Mwanasheria Mkuu na nafasi moja ni ya Mheshimiwa Spika.
Baraza la Wawakilishi linaendelea na Mkutano wake wa
Nne wa Baraza la Kumi na Moja, ambo ulianza tarehe 9 Septemba 2026.