Wawakilishi washiriki Bonanza la michezo Arusha.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar wameshiriki bonanza maalum la michezo jijini Arusha kwa kuonesha vipaji vyao katika michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu.

Wakizungumza wakati wa michezo hiyo iliyofanyika viwanja vya General tyre baadhi ya viongozi akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid wamesiaitiza umuhiku wa watanzania kutumia michezo kuimarisha afya na kuepukana na maradhi.

Ziara hiyo iliyowajumuisha Mawaziri, Manaibu Waziri na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni ziara ya kujenga mahusiano kati ya blw sport club na wazee arusha wazee sport club ambapo baadhi ya viongozi wa arusha sport club wamesema lengo ni kuimarisha zaidi mahusiano yaliopo.

Bonanza hilo lilishirikisha michezo mbalimbali ikiwemo riadha, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, na mengineyo ambapo washindi walipewa vikombe, medali na zawadi mbalimbali.