Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo ya BLW kutembelea maeneo ya kihistoria Mangapwani.

Posted on: 02.11.2026

Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo ya BLW kutembelea maeneo ya kihistoria Mangapwani.

Kamati Utalii, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeishauri wizara ya Utalii na Mambo ya kale kuboresha na kuimarisha miundombinu ya maeneo ya kihistoria ili kuongeza idadi ya watalii watakaotembelea maeneo hayo.

Kamati hiyo chini ya Kaimu Mwenyekiti Mhe. Said Ali Juma wamesema maeneo ya kihistoria ni mengi hivyo ni wajibu wa wizara kuyaimarisha na kuyaboresha Pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu uwepo wa maeneo hayo.

Wajumbe hao wamefafanua kuwa wizara inawajibu wa kutumia mitandao ya kijamii pamoja na watu wenye ushawishi wa kuyatangaza maeneo hayo ya kihistoria.

Waziri wa Utalii na Mambo ya kale Mhe. Nassra Nassor Omar amesema wizara inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuwapa mafunzo watendaji wa wizara ili kuboresha utendaji wa kazi zao.

Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo ilifanya ziara ya kutembelea maeneo ya kihistoria ikiwemo kisima cha chini kwa chini na Mahandaki ya watumwa Mangapwani.

 

// //