BARAZA LAPITISHA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027

Posted on: 19.06.2026
BARAZA LAPITISHA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027.
Wajumbe wa Baraza la wawakilishi wamekamilisha kuichangia Hotuba ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/27 na kupitisha kwa kauli moja jumla ya shilingi Trilioni 8.52.
Walipokua wakichangia katika mjadala wa hotuba iliyowasilishwa tarehe 11/06/2026, wajumbe hao wamesisitiza haja ya kutekelezwa vipaombele vilivyoanishwa katika bajeti hiyo ili iweze kuwanufaisha wananchi wote.
Baada ya Wajumbe kuridhika na hoja za Serikali Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe Juma Malik Akil amewashukuru wajumbe hao kwa ushirikiano wao na kuahidi kwamba serikali itahakikisha fedha zote zitatumika kwa uwazi na malengo yaliyokusudiwa.
Nae spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid amesema mjadala ulikua wa hoja na umesaidia kuboresha maeneo kadhaa katika makadirio ya serikali.
Maeneo yaliyopewa kipaombele katika bajeti hiyo inayoanza kutekelezwa rasmi tarehe 01 Julai ni pamoja na ujenzi wa miradi ya maendeleo, upatikanaji wa huduma za kijamii pamoja na uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi.