Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 18 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi

Posted on: 10.02.2025
Mkutano
wa Kumi wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya
Jumatano tarehe 12 Februari, 2025, saa 3:00 asubuhi.
A: SHUGHULI ZA BARAZA
Shughuli
za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-
1.
Maswali na Majibu.
Afisi
ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 190 kwa ajili ya
Mkutano huu.
2.
Miswada ya Sheria.
Miswada
ya Sheria iliyowasilishwa na kusomwa kwa mara ya Kwanza katika Mkutano wa mwezi
Disemba, 2024 itasomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa katika Mkutano huu wa
Kumi na Nane.
Miswada
yenyewe ni:-
(i)
Mswada
wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma, Nam. 11 ya
2016 na Kutunga Sheria ya Ununuzi wa Umma na Kuweka Masharti Bora ya Kusimamia
na Kudhibiti Ununuzi wa Umma na Mambo Mengine Yanayohusiana na HHHHHayo.
(ii)
Mswada
wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Baraza la Udhibiti wa Mfumo wa Utoaji Leseni za
Biashara, Nam. 13 ya 2013 na Kutunga Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Utoaji
Leseni za Biashara Zanzibar na Mambo Mengine Yanayohusiana na hayo.
3.
Uwasilishwaji
wa Ripoti za Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi kwa Mwaka 2024/2025.
4.
Taarifa
ya Serikali ya Mwelekeo wa Mpango wa Taifa 2025/2026.