Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 16 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi
Posted on: 09.09.2024
Mkutano
wa Kumi na Sita wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza
siku ya Jumatano tarehe 11 Septemba, 2024, saa 3:00 asubuhi.
SHUGHULI ZA
BARAZA:
Shughuli
za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-
1.
Maswali
na Majibu.
Afisi ya Baraza la Wawakilishi
imepokea na kuratibu maswali 280 kwa ajili ya Mkutano huu.
2.
Ripoti za Wizara
zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu utekelezaji wa Maagizo ya Kamati za Kudumu za Baraza kwa mwaka 2023/2024.
3.
Mswada
ya Sheria.
Mswada mmoja uliosomwa kwa mara
ya kwanza katika Mkutano wa Kumi na Tano utajadiliwa katika mkutano huu. Mswada
wenyewe ni:-
Mswada wa
Sheria ya Kuanzisha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo na Mambo Mengine Yanayohusiana
na Hayo.