CRDB yawakutaniusha Watunga Sheria katika Bonanza jijini Dodoma

Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeungana na timu ya Bunge la jamhuri ya muungano pamoja na vikundi mbali mbali vya michezo na mazoezi  katika bonanza CRDB BANK PAMOJA BONANZA lililofanyika Jijini Dodoma.

Bonanza hilo limeanza mapema asubuhi  kwa matembezi ya kilomita saba  ambapo spika tulia ackson aliyaongoza kupitia mitaa mbali mbali jijini dodoma na kumalizikia katika uwanja wa jamhuri jijini hapo.

Watunga sheria wa bunge na baraza la wawakilishi waliweza kushiriki katika michezo mbali mbali ikiwemo kuvuta kamba, mbio fupi, mpira wa pete na wengine kushiriki katika mchezo wa kulenga mishale.

Kivutio kikubwa katika bonanza hilo ni mpambano wa mpira wa miguu kati ya baraza la wawakilishi na bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania ambapo kwa bahati mbaya watunga sheria wa zanzibar walisalimu amri mbele ya kaka zao watunga sheria wa jamhuri baada ya kutunishiana misuli na kupelekea timu hizo kutoka sare ya goli moja kwa moja.

Kufuatia matokeo hayo muamuzi wa mchezo huo akalazimika  kuufanya mchezo huo uamuliwe kwa mikwaju ya penanti.

Jinamizi la kukosa penanti mbeba siwa faki suleiman kutoka baraza la wawakilishi  limepelekea timu ya bunge kulibakisha kombe la mashindano hayo katika makao makuu ya nchi huko dodoma kwa matokeo ya penanti sita kwa tano. [6 – 5]

Akizungumza mara baada ya kumalizika mchezo huo katibu wa baraza la wawakilishi sports club ambae pia ni mwakilishi wa jimbo la kikwajuni nassor salim jazira ameipongeza benki ya crdb kwa kuandaa mashindano hayo  na kuwaomba wachezaji wa timu ya baraza la wawakilishi kuendelea kujifua zaidi na mazoezi  ili kuweza kutwaa makombe katika mashindano wanayotarajia kushiriki hivi karibuni.

Mapema waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo  mhe tabia maulid mwita ameihakikishia timu ya baraza la wawakilishi kuendlea kuiunga mkono kwa ajili ya kusonga mbele katika mashindano ya ndani na yale ya  kimataifa kwa lengo la  kuirejesha heshima ya michezo zanzibar .

Meneja wa timu ya bunge seif khamis said ameuzungumzia mchezo huo kuwa ulikua ni mzuri na wenye ushindani mkubwa na kuiomba benki ya crdb kuandaa mashindano hayo upande wa zanzibar ili kuweza kuimarisha zaidi muungano uliopo.