Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid amewaongoza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika ziara ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha National Park jijini Arusha kwa madhumuni ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuvitangaza vivutio vya Utalii. Katika ziara hiyo Mhe. Spika ameambatana na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwemo baaadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri pamoja na wenyeji wao Arusha Wazee Sports Club.
Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Zubeir amesema Baraza la Wawakilishi limechukulia kwa umuhimu mkubwa tukio la uzinduzi wa filamu ya Royal Tour kwasababu ni hatua ambayo Mhe. Rais mwenyewe amechukua jukumu la kuileza dunia vitu vilivyopo Tanzania ili kuweza kutoa uwekezaji na masuala ya utalii katika kuongeza pato la Taifa.
Baadhi ya Wajumbe walioshiriki katika ziara hiyo wamesema wataendelea kuwa wazalendo katika kushirikiana na Serikali katika kuitangaza Tanzania katika maeneo yote yenye vivutio vya utalii pamoja na kuishauri vizuri Serikali njia nyengine zilizo bora za kuufungua utalii.
Nae Katibu wa umoja wa Arusha Wazee Sports Club George Kessy ameushukuru na kuupongeza uongozi wa Baraza la Wawakilishi kwa kuendeleza kwa vitendo ushirikiano uliopo baina ya pande hizo mbili, Maeneo waliotembelea katika hifadhi hiyo ni turisia Water fall, Serengeti ndogo, pamoja na kuangalia wanyama.