Taarifa ya shughuli za Mkutano wa Nane wa Baraza la Kumi la Wawakilishi

Mkutano wa Nane wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku
ya Jumatano tarehe 07 Septemba, 2022, saa 3:00 asubuhi.

A: SHUGHULI ZA BARAZA:
Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-

 1. Maswali na Majibu.
  Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 159 kwa ajili ya Mkutano huu.
 2. Miswada ya Sheria.
  Miswada miwili ya Sheria itawasilishwa na kujadiliwa, Miswada yenyewe ni:-
  i. Mswada wa kufuta Sheria ya Baraza la Wawakilishi (Kinga, Uwezo na
  Fursa), Nam. 4 ya 2007 na kutunga Sheria mpya ya Baraza la Wawakilishi
  (Kinga, Uwezo na Fursa) katika kutekeleza kazi na mambo mengine
  yanayohusiana na hayo.
  ii. Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na
  Washauri Elekezi wa Kodi Zanzibar na mambo mengine yanayohusiana na
  hayo.
 3. Kauli ya Serikali Kuhusiana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
  kwa Mwaka wa Fedha Unaoishia Tarehe 30 Juni, 2021.
 4. Ripoti za Wizara zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu utekelezaji wa
  Maoni, Ushauri na Mapendekezo ya Kamati za Kudumu za Baraza kwa mwaka
  2021/2022.
 5. Taarifa ya Serikali (Taarifa ya Mchezo wa Ngumi – Zanzibar).
 6. Miswada kusomwa kwa mara ya kwanza: