Spika aahidi mashirikiano kwa Kamati ya haki na usawa
Kamati ya
ushauri ya kitaifa ya haki na usawa wa kiuchumi kwa wanawake imeandaa program
ya kuwasaidia wanawake hapa nchini yenye lengo la kuondekona na changamoto za
kijamii na kiuchumi katika sekta tofauti ikiwemo elimu na ajira.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo Bi Angellah Kairuki amesema hayo katika Afisi za Baraza la Wawakilishi
wakati Kamati ikijitambulisha kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir
Ali Maulid.
Bi Angellah
amesema proramu hiyo inalenga utekelezaji wa maazimio ya yaliyofikiwa kufuatia
mikutano iliyofanyika nchini Mexico, Beijang na Umoja wa Mataifa ni kumuinua
mwanamke katika sekata mbalimbali za kijamii na kiuchumi na kumpatia fursa za
kiamendeleo.
Nao Wajumbe
wa Kamati hiyo wameahidi kusimama pamoja kumuunga mkono Mheshimiwa Raisi wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha jambo hili linafanikiwa.
Spika wa Baraza
la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali mMauldi amesema watatoa ushirikiano wa
kutosha kwa kamati hiyo ikiwemo kuitambulisha kwa wajube wa baraza la
wawakilishi ili lengo lililokusudiwa liweze kufikiwa.