HOUSE OF REPRESENTATIVES

BARAZA LA WAWAKILISHI

News from the House

Wajumbe BLW waipiga Jeki Zanzibar Heroes

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wametoa jumla ya  shilingi  10,875,000 /=  (Milioni Kumi laki Nane na Sabini na Tano Elfu)  kwa ajili ya kuichangia timu ya  Taifa ya  Zanzibar Zanzibar Heroes ambayo kwa sasa iko nchini Kenya kushiriki mashindano ya Challenge.

Kiasi hicho cha fedha kinatokana na kila mjumbe kuchangia shilinngi  Laki Moja na Ishirini na Tano Elfu  125,000/=  ambapo kiasi kikubwa cha Fedha hizo wameshatumiwa wachezaji kwa ajili ya kujikimu na masuala mengine ya kimichezo huko waliko.

Aidha, asilimia ndogo sana ya mchango huo itatumika kwa ajili ya mapokezi na tafrija ya pamoja itakayowajumuisha pia na Waheshimiwa wajumbe ambayo itakayofanyika katika Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwana baada ya kurejea hapa nchini.

Akizungumzia mchango huo, Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo , Mhe. Rashidi Ali Juma, amesema  Baraza  la wawakilishi  hadi hivi sasa ni taasisi ya mwanzo kuchangia kiasi kikubwa cha fedha kwa timu hiyo.

Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes hivi sasa iko nchini Kenya kushiriki katika Mashindano ya Challenge na tayari imefuzi katika hatua ya nusu fainali.


Hon. Zubeir Ali Maulid (Speaker)

Upcoming Events

Stay connected