WIZARA YA TAWALA ZA MIKOA YASHAURIWA KUJENGA MAJENGO YA MAKAO MAKUU.

Posted on: 11.05.2026

Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeishauri  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ kuandaa mipango itakayoibua miradi ya ujenzi wa majengo ya makao makuu ya wizara.

Kamati imetoa ushauri huo baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ kuwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Mapato kwa Mwaka wa fedha 2026/2027 katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.

Kamati imesema kuibuliwa kwa miradi ya ujenzi kwa wizara hiyo kutasaidia kupunguza changamoto uhaba wa Ofisi na kukidhi mahitaji ya watumishi.

Aidha Kamati imebaini tatizo la kutoonekana kwa mapato yaliyopangwa kutoka Hazina kwa mwaka wa fedha 2026/2027 licha ya kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amewaomba Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuidhinisha matumizi ya shilingi 695,735,989,000/=  na mapato ya shilingi 8,817,956,000/= kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

//