Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuimarisha Afya na Usalama kazini

Posted on: 26.11.2026

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kuanzishwa kwa sheria mpya ya Usalam na Afya kazini itasaidia kuhakikisha usalama, afya na ustawi wa watu dhidi ya hatari zitokanazo na shuhuli za kazi.

Akiwasilisha Mswada wa kuanzishwa kwa Sheria hiyo katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Tano wa Baraza la Kumi na Moja la Wawakilishi kilichoanza leo waziri wa kazi, ajira, vijana na uwezeshaji Mhe. Ali Suleiman Ameir amesema kuwepo kwa sheria hiyo pia kutaanzisha mamlaka ya kisheria itakayosimamia masuala ya usalama katika sehemu za kazi.

Ameshauri kuwa mamlaka hiyo iwe na mpango endelevu wa kutoa elimu katika taasisi za serikali na binafsi juu ya umuhimu wa usalama na afya  kazini.

Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Uwezeshaji Mhe. Makame Mohammed Sufiani ameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwepo kwa sheria hiyo.

// //