Taarifa ya shughuli za Mkutano wa 10 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi

Posted on: 13.02.2023

Mkutano wa Kumi wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 15 Februari, 2023, saa 3:00 asubuhi.

A: SHUGHULI ZA BARAZA

Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-

1. Maswali.

Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 170 kwa ajili ya Mkutano huu.

2. Uwasilishwaji wa Ripoti za Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi kwa mwaka 2022/2023.

3. Miswada wa Sheria.

Mswada mmoja ambao ulisomwa kwa mara ya kwanza katika kikao kilichopita, utasomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa katika kikao hiki; mswada huo ni:-

“Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo".

4. Taarifa ya Wabunge watano (5) wanaoliwakilisha Baraza katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.

5. Ripoti ya Mapendekezo ya Muelekeo wa Mpango wa Taifa.

//