UNDP, Kuimarisha Mpango wa Awali wa kuanzisha Mradi (IPP), kuendeleza mradi wa muda mrefu wa kulijengea uwezo Baraza la Wawakilishi Zanzibar

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo la UNDP, limesema limeimarisha Mpango wa Awali wa kuanzisha Mradi (IPP), ambao unalenga kuendeleza mradi wa muda mrefu wa kulijengea uwezo Baraza la Wawakilishi Zanzibar (Zan LSP)

Wataalam wa Mradi kutoka Shirika hilo wakiwemo (Paul Mlemya,mtaalam katika masula ya ufuatiliaji na Tathmini na Fridah Mwakasyuka ,mtaalam Programu) wamesema tayari Mpango huo umeainisha activities mbali mbali kwa maandalizi ya mradi huo ambao pia utaendeleza activities za mradi uliopita (LSP II) ambao pia unatekelezwa Tanzania Bara.

Wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo  baadhi ya watendaji wa Baraza ambao ni Timu ya kuratibu mradi wa  (Zan LSP)utakapoanza rasmi,wataalamu hao wamesema activities nyengine katika mpango huo wa awali ni pamoja na kupata ushauri kutoka wa wadau mbali mbali zikiwemo Jumuiya zisizo za serikali hasa za Wanawake,Vijana,Utafiti pamoja Taasisi za kitaaluma juu ya namna bora ya kuzijengea uwezo ili ziweze kushiriki katika kusaidia Mabunge likiwemo Baraza la Wawakilishi kutekeleza majukumu yao katika misingi ya kidemokrasia .

Wamefahamisha kuwa Mpango huo unakusudia kuwajengea uwezo wajumbe wapya wa Baraza la Wawakilishi waliochaguliwa katika kipindi cha 2020-2025 ili Baraza liweze kuwa taasisi bora ya kidemokrasia kwa ajili ya maendeleo ya ustawi wa watu wa Zanzibar kama ilivyoainishwa katika Mpango Mkakati wa Baraza wa mwaka 2021-2025, Sheria mbali mbali pamoja na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010.

Mafunzo kuhusu Mpango wa Awali wa kuanzisha Mradi (IPP), ambao unalenga kuendeleza mradi wa muda mrefu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) wa kulijengea uwezo Baraza la Wawakilishi Zanzibar (Zan LSP), yalifanyika katika hoteli ya Ngalawa nje kidogo na mji wa Zanzibar .

Mada tofauti zilijadiliwa zikiwemo Usimamizi wa Mradi,Ufuatiliaji na Tathmini,Uzingatiaji wa thamani ya Fedha katika Miradi (Value for Money) pamoja na umuhimu wa  kuwa na Miradi inayozingatia matokeo.

Tokea mwaka 2010 -215, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP limekuwa na Mradi wa kulijengea uwezo Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mradi huo ulisita kwa upande wa Zanzibar kutokana na sababu mbali mbali. Hata hivyo Shirika hilo hivi sasa limeonesha nia la kuurejesha tena mradi huo ambapo kwa hatua za awali tayari limekuwa na Mpango wa awali kuelekea kuwa na Mradi mkubwa wa miaka mitano ambao  unaotarajiwa kuanza mwaka 2023.