HOUSE OF REPRESENTATIVES

BARAZA LA WAWAKILISHI

News from the House

Mamadou Sakho wa Crystal Palace atembelea Baraza la Wawakilishi

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na Timu ya Crystal Palace ya Uingereza Mamadou Sakho ametembelea Baraza la Wawakilishi kwa lengo la kuona shughuli za chombo hicho cha kidemokrasia hapa Zanzibar.

Sakho  akiwa amefuatana  na mkewe wake Majda Sakho alielezea kufurahishwa kwao na mapokezo mazuri waliyopata pamoja  na kuwaomba watu wengine maarufu kutembelea chombo hiki.

Sakho yupo hapa Viswani Zanzibar kwa ziara ya kiutalii na mapumziko ya mwisho wa msimu wa ligi kuu ya Uingereza iliyomalizika hivi karibuni.


Hon. Zubeir Ali Maulid (Speaker)

Upcoming Events

Stay connected