Spika aahidi Mashirikiano kwa Kamati ya Haki na Usawa

Kamati ya ushauri ya kitaifa ya haki na usawa wa kiuchumi kwa wanawake imeandaa program ya kuwasaidia wanawake hapa nchini yenye lengo la kuondekona na changamoto za kijamii na kiuchumi katika sekta tofauti ikiwemo elimu na ajira.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Bi Angellah Kairuki amesema hayo katika Afisi za Baraza la Wawakilishi wakati Kamati ikijitambulisha kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid.

Bi Angellah amesema proramu hiyo inalenga utekelezaji wa maazimio ya yaliyofikiwa kufuatia mikutano iliyofanyika nchini Mexico, Beijang na Umoja wa Mataifa ni kumuinua mwanamke katika sekata mbalimbali za kijamii na kiuchumi na kumpatia fursa za kiamendeleo.

Nao Wajumbe wa Kamati hiyo wameahidi kusimama pamoja kumuunga mkono Mheshimiwa Raisi wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha jambo hili linafanikiwa.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali mMauldi amesema watatoa ushirikiano wa kutosha kwa kamati hiyo ikiwemo kuitambulisha kwa wajube wa baraza la wawakilishi ili lengo lililokusudiwa liweze kufikiwa.